Skip to main content

Hivi majuzi, kundi la wanawake viongozi walikusanyika kwenye warsha muhimu, ili kuchangia mabadiliko, kueneza maarifa, na kwa pamoja kupanga mikakati ya uongozi bora wa wanawake katika kaunti za eneo la Pwani zikiwemo Tana River, Taita Taveta, Kilifi, Kwale, Lamu, na Mombasa.

Warsha yenyewe iliandaliwa na shirika la Echo Network Africa Foundation, wakishirikiana na Hanns Seidel Foundation Kenya.

Kwa muda mrefu sana, wanawake wamekuwa na michango yenye thamani, ila imekuwa ikiwakilishwa kidogo tu katika nafasi za sekta nyingi zinazounda jamii zetu.

Ingawa tumeona hatua zilizopigwa, safari ya kuafikia uongozi wenye usawa kwa wanawake katika maeneo kama vile biashara, huduma za afya, elimu, kilimo, na utawala wa mitaa katika eneo la Pwani bado ina changamoto kubwa.

Warsha hii ilipatiana jukwaa muhimu la kutathmini kwa uwazi pale tunaposimama na, muhimu zaidi, pale tunapotamani kuwa.

Barabara ya uongozi ni mara chache hukosa vikwazo. Wanawake, hasa, mara nyingi hukabiliana na vikwazo vya kipekee— viwe kanuni za kitamaduni, matarajio ya jamii, kutofikia ifaavyo rasilimali na mitandao, au suala lililoenea la upendeleo wa jinsia moja.

Vizuizi hivi vinaweza kukandamiza tamaa ama hamu, na kuzuia hata watu wenye maarifa kufikia uwezo wao kamili katika uongozi na majukumu ya uongozi.

Hata hivyo, si yote tu kuhusu vikwazo; pia kuna nafasi kubwa sana.

Kuongezeka kwa kutambua thamani ya uongozi mbalimbali na tofauti, kuenea kwa mtandao wa wanawake waliowezeshwa, na masharti ya kikatiba ya usawa wa kijinsia; yote yanaleta sababu nzuri ya maendeleo.

Sehemu muhimu ya mjadala katika warsha ilikuwa inaimarisha harakati na sauti za wanawake, hasa tunapoangalia mpangilio wa uchaguzi ujao.

Nguvu zao za pamoja zipo katika uwezo wao wa kujipanga, wa kueleza maswala yanayowahusu na wanayoyapa kipaumbele, na kutetea maswala ambayo ni muhimu sana kwo na kwa jamii zao.

Iwe ni kutetea huduma bora za afya, miundombinu iliyoboreshwa, uwezeshaji wa kiuchumi, au ulinzi wa mazingira; sauti zao zikiwa zimeunganishwa zinaweza kuwa nguvu kubwa sana ya mabadiliko.

Ni muhimu waweke mikakati ya jinsi ya kujihusisha vilivyo na kalenda au ratiba ya uchaguzi, wakihakikisha kwamba maswala ya wanawake yapo mstari wa mbele katika ajenda za sera.

Na hatimaye, lakini labda muhimu zaidi, warsha hii ilitoa nafasi ya kubadilishana uzoefu.

Kila mmoja wa wahusika alibeba hadithi ya kipekee, safari ya kipekee, iliyojaa ushindi na changamoto za kipekee. Zikijumuishwa, ufahamu wao, uthabiti wao, na hekima yao ilikuwa ni muhimu sana.

Kulikuwa na hali ya uwazi na kuaminiana, ambapo wahusika waliweza kuelezea uzoefu wao kwa uhuru, kujifunza kutoka kwa mafanikio na vikwazo vya mwanamke mwingine, na kuunda mtandao thabiti, wenye uwezo wa kuungana mkono zaidi.

Warsha sawia ilifanyika awali katika mji wa Meru, ikiwaleta pamoja wanawake viongozi kutoka kaunti za Meru, Tharaka Nithi, Isiolo, na Embu.

Ni katika kushiriki kwenye simulizi kama hizi ndipo wanawake wanapata hoja zinazofanana, wanapata msukumo, na kuimarisha azimio la pamoja la uongozi.

Robertson Kabucho
Head of Programmes, Kenya & Ethiopia, Hanns Seidel Foundation